MSHENGA ASO NA MAANA YOYOTE.

July 22, 2018

Ambokile kijana wa kinyakyusa toka Mbeya alikuwa akijishughulisha na kazi za kugonga kokoto maeneo ya Kimbiji Kigamboni,shughuli hii aliianza miaka mitano iliyopita kiasi ambacho ilimfanya azoeleke sana maeneo yale.

Ambokile akiwa na wagonga kokoto wenzie majira ya mchana walikuwa wakila kwa mama ntilie .

Siku moja Ambokile akiwa na wenzie walikwenda kula kwenye banda la mama Sikitu Ambokile alivutiwa na binti mmoja aliyekuwa akimsaidia mama Sikitu kuwahudumia wateja, Ambokile alitafuta mwanya akamtamkia binti yule jinsi anavyompenda!

Binti yule aliyekuwa kajifunga ushungi muda wote alimwambia apeleke barua kwao ili amuoe.Ambokile akaridhia akatafuta mshenga barua ikaandikwa na soon majibu yakatoka,Moja ya masharti ilitakiwa Ambokile asilimu,Kwakuwa alishapenda alitekeleza yote.

Mambo yakaenda sawia Ambokile akawa ameshapata jiko huku akiitwa AbdulKareem baada ya kubadili dini!

Ambokile aliendelea kufanya kazi yake huku akimpenda na kumtimizia mahitaji mkewe kadiri awezavyo!Ila alikuwa akishangaa mara nyingi watu walikuwa wakinong’ona kila wanapomuona hali ambayo haikuwepo kabla!Siku zilipita kwa kasi siku moja Ambokile alienda kazini kwake ila hali yake kiafya haikuwa vzr sana!

Kwahyo alipoona hajisikii vizuri ikamlazimu arudi nyumbani kwake,alifika nyumbani kwake mapema tu ikawa surprise kwa mkewe!

Cha kushangaza mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani halafu aliona viatu vya kiume nje,

Ambokile alinyata mpaka dirishani akachungulia chumbani na kumuona mshenga na mkewe wakiwa uchi wa mnyama wakifanya yao!Ambokile aliumia sana huku akimsikilizia mkewe akigugumia kimahaba.

Kinachoumiza zaidi mshenga alizoeleka kuja pale akiwashauri jinsi ya kuishi vema katika ndoa,ila majirani nahisi walishagundua kitu!

Ambokile alikusanya nguvu na kuurukia mlango kwa nguvu na kuuvunja!Mkewe na mshenga walishikwa na fadhaa wakataka kukimbia!

Ambokile alichukua panga lililokuwa jirani na kutaka kuwakatakata, Kama ujuavyo uswahilini watu walishajaa! Mshenga kafumaniwa ilikuwa habari kubwa mtaa huo. Bahati nzuri watu waliwahi kumkamata Ambokile kabla hajafanya kitendo chochote.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 + three =