Mimi na Mama Omba Omba.

July 22, 2018

Kuna siku wakati nasoma Chuo nilipoteza Wallet yangu ambayo ilikuwa na fedha zote za matumizi. Nilijisikia vibaya sana. Alafu ilikuwa siku ambayo Chuo tuna TEST so wakati naelekea kituo cha Daladala Walllet ikadondoka.

Wakati nataka kuingia kwenye gari nikagundua sina Wallet, ikabidi nirudi chap kuicheki huenda nimeidondosha au nimesahau nyumbani. Njiani sikuipata nikaenda moja kwa moja ghetto sikuikuta. Nilihuzunika mno.

Licha ya kuwa na hela yangu ya matumizi, lakini kulikuwa na hela za wana ambao tulikuwa tumechanga kwa ajili ya kwenda kuwatembelea wagonjwa Hospitalini. So nazo zikapotea. Ilikuwa kama 100K. Nayo ikaenda.

Ilibidi nichape Hamza Kanuni mpaka Chuo. Wakati natembea nikawa nawaza mengi na kuona kama dunia nzima imenielemea. Nikahisi kama Mungu amenisahau na kunitwisha mzigo mzito ambao nisingeweza kuumudu.

Nilipofika kati kati ya Jiji maana Chuo nilichosoma kilikuwa katikati ya Jiji (CBE ), Nikamkuta Omba omba mmoja mwanamke akiwa ameketi chini, anaomba msaada. Sikuwa na hata mia ila nilijikuta nakaa chini kuzungumza nae.

Alinieleza aliyoyapitia (HIYO NI STORY NYINGINE) mpaka kuwa katika hali kama ile ambayo mkono wake wa kulia haukuwa na vidole, Sura imeungua ungua  na mguu mmoja umeshakuwa kilema. Wanangu watu tunaonana na kuishi pamoja ila sisi ni wabaya sana.

Alivyomaliza kunisimulia nilitoa machozi na sikuwa na maumivu ya kupoteza wallet yangu hata kidogo zaidi ya kuwaza hali ya mama yule. Nilijisemea “Najiona nina matatizo kumbe kuna watu hawawezi hata kutembea au hata kufanya ninayoyafanya mimi, na bado hawamlalamikii Mungu”.

Ilibidi nimuage niwahi kufanya Tes. Nilizoea kuwa napita kila siku namuachia nilichokuwa nimebarikiwa na wakati mwingine tunapiga stori yaani akawa kama rafiki yangu. Nikabahatika kuwafahamu baadhi ya ndugu zake waliokuwa mkoani. Ambao baada ya matatizo walimkataa.

Siku moja naenda kufanya mtihani  sikumkuta alipokuwa na nilitaka nipite maksudi tuombe hata dua mbili tatu, SIkumkuta. NIkaenda nikachapa paper. Baada ya siku mbili ndugu zake nikawasiliana nao wakasema alifariki kuna gari lilimgonga.  “Inna lillahi wa inna ilaihi raji’un”

Nikawa nayakumbuka baadhi ya maneno yake ambayo aliwahi kuniambia. “Mwanangu katika maisha haya kila jambo lako mtegemee Mungu pekee maana yeye ndo mkuu wa kila kitu”.

“Haijalishi wanadamu wanasema nini juu yako, au wanakuzushia nini, ukijieleza wasipokuelewa muachie Mungu. Wakikufanyia ubaya kama walionifanyia mimi muachie Mungu, atakulipia”.

“Mwanangu, Mshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai na uzima wa afya anaokubariki, unakutana na watu wengi barabarani kila mtu ana yake, wengine wana mengi zaidi yako wewe”.

“Mwanangu, isitokee hata siku moja ukawa mlalamishi kwa muumba wako kwa sababu tu ya matatizo unayopitia, piga goti muombe, akikunyima mshukuru akikupa mshukuru pia, huo ndio msingi mzuri”.

“Mwanangu sio kila omba omba unayemuona barabarani anahitaji pesa, wengine wanahitaji faraja na watu wa kuwasikiliza matatizo yao, hata wasipoweza kuyatatua ila tu wawasikilize na kuwafariji” Faraja ina nguvu sana.

“Katika maisha mthamini kila mtu hata kama kuna kitu unamzidi, maana aliyekupa akiamua kukichukua hicho kitu ni sekunde”. Aliniambia mengi ambayo kwa leo nimependa kukushirikisha na wewe unayesoma hii stori fupi, Ikikupendeza mpasie na mwenzako huenda akawa na cha kumfaa yeye.

Kila siku pigeni goti na kusali na kumshukuru Mungu kwa neema ya uhai anayokupa ndugu yangu. Wapo wengi ambao wanataabika sana huko. Kama huamini tenga muda wako siku moja toka, nenda Hospitali au hata Magereza ya Wafungwa pata muda wa kuzungumza nao. Kuna mengi utafahamu.

Maisha ni kuishi, Furahia maisha. Hakikisha unaishi katika misingi mizuri ambayo haimkasirishi mtu yoyote na haimkasirishi Mungu. Tenda wema pekee duniani kwa watu wote bila kuwawekea matabaka wala nini. Maana mbora mbele za Mungu ni mcha Mungu pekee.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

thirteen − 11 =