MCHUMBA.

July 22, 2018

Msichange na kununua gari lenu mkiwa wachumba

Msichange na kununua shamba, kiwanja au nyumba yenu mkiwa wachumba.

Msianzishe biashara ya pamoja mkiwa wachumba.

Msikopeshane kiwango kikubwa cha pesa mkiwa wachumba.

Msishirikiane kukopa kiwango kikubwa Bank au kwenye taasisi za fedha mkiwa wachumba.

Haishauriwi kabisa kwa watu ambao ni wachumba kushirikiana kifedh na mipango iliyotajwa hapo juu wakati wakiwa ni wachumba. Mambo hayo hapo juu yanapaswa yafanywe na watu ambao tayari ni wanandoa.

Uchumba sio ndoa, hauna “garantee” wala hauna mashiko. Unaweza kuvunjika dakika yoyote ile na kama mlikuwa mmesha wekeza kila mmoja kwa mwenzake kwa kuamini kwamba si mtakuja kuoana, uzoefu unaonyesha kwamba mara nyingi mmoja kati ya wachumba hao ambaye mali ilikuwa imeandikishwa kwa jina lake huishia na mali ile na kumdhurumu mwenzake bila kujali kwamba mali hizo walikuwa wamechanga wote wawili wakati ule wa mapenzi moto moto na kuacha jeraha na maumivu makubwa sana kwa mmoja aliyedhurumiwa kitu ambacho kama hakitashughulikiwa vizuri katika ushauri “counseling” huweza kuleta athari za kimahusiano kwa mchumba atakayefuata na hata mwanandoa atakaye oana naye ataumizwa kwasababu ya lile jeraha la kudhurumiwa ambalo mchumba alitoka nalo kule.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

18 − 15 =