Fahamu App ya ‘SIKILIZA’ yenye uwezo wa kusikiliza radio zote duniani

January 8, 2018

Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele na ukuaji wa Teknolojia unazidi kupiga hatua ambapo vijana duniani kote wamekuwa wakipambana kubuni bidhaa mbalimbali za kielekroniki.

Habari nzuri ni kwamba kuna App nzuri ya kiswahili ambayo inafahamika kwa jina la “SIKILIZA” ambayo imetengenezwa na Watanzania yenye uwezo wa kusikiliza Redio yoyote ukiwa sehemu yoyote kwa urahisi zaidi.

App hii inapatikana kwa watumiaji wa Android kupitia Google Play Store ambako unaweza kupakua na kusikiliza Radio za Tanzania, DR Congo, Uganda na Kenya kwa sasa lakini baadae itakuwa na uwezo wa kupatikana kwa radio zote duniani.

Hata hivyo App hii ni ya tofauti na nyingine kwani unaweza kuingia kwenye website yake ya (sikiliza.co.tz) ambapo pia unaweza kusikiliza radio zote za TanzaniaKenyaUganda na DR Congo, Ingawa kuna baadhi ya nchi bado hazijawekwa lakini zitaongezwa hivi karibuni.

Uzuri ni kwamba App ya ‘SIKILIZA’ ipo tofauti na App nyingine tulizozizoea kuzitumia kwani radio zote zimewekwa katika mtiririko wa mikoa  ambako radio unayoitaka kuisikiliza inapatikana.

Urahisi mwingine ni kwamba App hii haina size kubwa na ni nyepesi kufunguka na inakubali kutumia mfumo wa 3G, 4G na Wi-Fi , kwa hiyo kwa wewe  mwenye simu yenye size ndogo haina haja ya kuogopa kuipakua.

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!